News

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Katika kuongeza nguvu kwenye jitihada za Serikali za kupambana na magonjwa ya milipuko katika vituo vya kutolea huduma za afya na jamii, Taasisi ya Benjamin William Mkapa kwa kushirikiana na Serikali ilifanikiwa kupata ufadhili kutoka kwa wadau wa maendeleo kuajiri wataalamu wa afya 593 na kufanya kazi na Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii 1,630. Ajira hizi ni za mkataba wa miezi sita kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2020 kwa wataalamu wa afya na miezi mitatu kwa watoa huduma za afya ngazi ya Jamii. Watumishi hawa wamekua wakitoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya na katika jamiii ndani ya Wilaya 70 na Mikoa 22.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, ajira hizi za dharura zilikua ni kwa kipindi cha miezi sita tu kama ilivyoainisha katika mikataba ya ajira ya watumishi hawa. Mikataba hii haikuwa na kipengele cha kuendeleza kipindi cha mkataba wala kuhuwishwa katika utumishi wa umma baada ya kukamilika kwa kipindi hiki cha mkataba.

Taasisi itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kutatua uwepo wa wataalamu wa afya na watoa huduma za afya katika Jamii, na pale itakapotokea uwezo na nafasi ya kuendeleza ajira hizi za dharura, watumishi wote waliomaliza mikataba yao chini ya afua hii watafahamishwa na kupewa kipaumbele.

IMETOLEWA NA TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Leave a Reply

Facebook

Twitter