Nukuu za Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kilele cha maadhimisho ya kumbukizi ya urithi wa Hayati Benjamin Willliam Mkapa.
“Tunapongeza na kutambua jitihada za Taasisi ya Mkapa kupitia mpango wake wa Mkapa Fellows ambao umewezesha wataalam wa afya takribani 7322 kupata ajira ya mpito wakati wakisubiri ajira rasmi. Asilimia 37% ya waajiriwa hawa wa mpito baadae wameajiriwa na Serikali kwa ajira za kudumu. Napenda kuwahakikishia Taasisi ya Mkapa na wadau wengine kuwa, kadri serikali itakapotoa ajira, basi hao watalaam wa afya wa Mkataba (Mkapa fellows) wataendelea kuhuishwa katika ajira za serikali. Naelekeza Ofisi ya Rais Utumishi kuzingatia hili katika vibali vya ajira ambavyo vya kuajiri watumishi wa afya ambavyo tumetoa kwa mwaka 2024/2025 kwa wale watakaotimiza vigezo.” alisema Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan.