Hotuba za Viongozi katika maadhimisho ya kumbukizi ya urithi wa Hayati Benjamin William Mkapa

Nukuu za Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kilele cha maadhimisho ya kumbukizi ya urithi wa Hayati Benjamin Willliam Mkapa.

“Tunapongeza na kutambua jitihada za Taasisi ya Mkapa kupitia mpango wake wa Mkapa Fellows ambao umewezesha wataalam wa afya takribani 7322 kupata ajira ya mpito wakati wakisubiri ajira rasmi. Asilimia 37% ya waajiriwa hawa wa mpito baadae wameajiriwa na Serikali kwa ajira za kudumu. Napenda kuwahakikishia Taasisi ya Mkapa na wadau wengine kuwa, kadri serikali itakapotoa ajira, basi hao watalaam wa afya wa Mkataba (Mkapa fellows) wataendelea kuhuishwa katika ajira za serikali. Naelekeza Ofisi ya Rais Utumishi kuzingatia hili katika vibali vya ajira ambavyo vya kuajiri watumishi wa afya ambavyo tumetoa kwa mwaka 2024/2025 kwa wale watakaotimiza vigezo.” alisema Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan.

Nukuu za Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Msarifu wa taasisi ya Mkapa Foundation katika kilele cha maadhimisho ya kumbukizi ya urithi wa Hayati Benjamin Willliam Mkapa.

“Kuwepo kwa Mkapa Fellows idadi ya 7,322 leo hii, ambapo asilimia 37% wameajiriwa Serikalini na waliobakia wapo chini ya miradi ya Taasisi na katika Sekta Binafsi, ni ushahidi wa jinsi Hayati Rais Mkapa alivyowekeza nguvu zake katika kuimarisha sekta ya afya.” alisema Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi.

Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua rasmi mkutano wa kitaifa wa Rasilimali Watu katika Sekta ya Afya tarehe 30 Julai 2024.

Benjamin William Mkapa Health Plaza | Plot No. 2006, Turi Road (off Mwai Kibaki Rd), Mbezi Beach Kawe, Dar Es Salaam

Mon – Thur: 8:00 am – 5:00 pm

Fri: 8:00 am – 13:30 pm

Benjamin Mkapa Foundation © 2024. All Rights Reserved